Madina
Issa na Khamisuu Abdallah
MTOTO
wa kiume anaekisiwa kuwa na umri wa miaka sita mkaazi wa Bambi, amepigwa na
baba yake kwa kitu kizito na kumsababishia maumivu makali.
Akizungumza
na waandishi wa habari hizi, Daktari wa kitengo cha mkono kwa mkono cha
hospitali kuu ya Mnazimmoja, Salum Omar Mbarouk, alithibitisha kumpokea mtoto
huyo na kusema dalili zinaonesha alivunjika.
Alisema
baada ya kumpokea alimpima na kugundua kuwa mtoto huyo alipigwa na kitu kizito
kilichomsababishia kuvunjika.
Aidha
alisema mtoto huyo baada ya kupelekwa katika mashine ya kuchunguza mifupa
(x-ray) ilionesha mtoto alivunjika na tayari ameshaanza kupatiwa matibabu.
Hivyo
alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao kwani hao ndio
tegemeo la baadae.
Aliitaka
jamii inapowaokota watoto kama hao wanaofanyiwa udhalilishaji kuripoti kituo
cha polisi ili sheria iweze kuchukua hatua zaidi.
“Baba
yake ana tabia ya kumuacha mtoto wake nyumbani ambapo huondoka na mtoto wake wa
kike sasa huyu huondoka na kwenda kiambo cha juu kwa ajili ya kucheza lakini
akirudi huchezea kipigo,” alisema Mratibu wa wanawake na watoto, Mashavu
Ramadhan Abdallah,.
Alisema
mtoto huyo alimuona kwa bibi ambae alimuhifadhi baada ya kumuona anapigwa.
Sambamba
na hayo Mratibu huyo alisema baba huyo ni mzoefu wa matukio ya udhalilishaji
kwani alimtahiri mtoto Gumba kwa kutumia kisu huku dawa ikiwa pombe ya
kienyeji.
“Baba
yake huyu mtoto anaonesha kuwa ni katili sana kwani alimtahiri kwa kisu na
pombe ya kienyeji kufanywa ndio dawa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment