YA FASIHI YA KIAFRIKA
Tangazo la Washindi
Washindi wa tuzo mpya ya
Mabati-Cornell ya Fasihiya Kiafrika walitangazwa leo (Novemba 17, 2015).
Lengo kuu la tuzo hii ni kutambua uandishi bora kwa lugha za Kiafrika na kuhimiza tafsiri kutoka lugha za Kiafrika
kwa lugha nyingine, baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe, na pia kwa lugha
za Kiafrika.
Washindi wa kwanza wa tuzo hii ni:
Zawadi ya Kwanza yaRiwaya - $5,000:
Anna Samwel Manyanza kwa Penzi la Damu
Zawadi ya Kwanza yaUshairi - $5,000:
Mohammed K. Ghassanikwa N'naKwetu
Zawadi ya Pili katika utanzu wowote
- $3,000: Enock Maregesikwa KoloniaSantita
(riwaya)
Zawadi ya Tatu katika utanzu wowote,
$2,000: Christopher Bundala Budebah kwa Kifaurongo
(ushairi)
Hiyo ni miongoni mwa miswada 65
iliyowasilishwa, na kusomwa na waamuzi 6:
Riwaya - Dk. Farouk Topan, Prof.
Sheila Ryangana Prof. Mohamed Bakari.
Ushairi - Bi. Rukiya Harith Swaleh,
Prof. Clara Momanyina Prof. Alamin Mazrui.
Waamuzi walisema kuwa, “ Wakitumia lugha
inayovutia na iliyo muwafaka, na mara nyingine lugha cheshi, washindi walizungumzia
maswala yanayozikumba jamii zaAfrika Mashariki, kama vile utumiaji wa mihadharati
na athari zake duniani; swala la jinsia – wanawake na haki zao; na ufisadi wa kisiasa.
Huu ni ukweli halisi wa Afrika katika lugha ya Kiafrika.”
Washindi watakabidhiwa zawadi zao katika Tamasha
la Fasihi la Kwani?(Kwani? Lit Fest) litakalofanyika Desemba
3, 2015 katika Klabu ya Capital mjini Nairobi, Kenya.
Sarit Shah, Mkurugenzi wa Mabati Rolling Mills
Kenya alisema, “Kuongezeka kwa matumizi ya Kiswahili kuwa ni lugha kuu ya mawasiliano
Afrika Mashariki hakuwezi kupuuzwa. Tunaamini kuwa lugha na tamaduni huboresha mahusiano
ya kikazi na yakibinafsi. Hapa Safal, hasa hapa Mabati, tunajivunia kuwa katika
jamii hii inayoendelea kukua.”
Abdilatif Abdalla, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini,
alisema, “Jambo la kufurahisha ni kwamba sehemu kubwa ya miswada iliyopokewa ilikuwa
ni ya kiwango cha juu. Kwasababu ya kanuni za tuzo hii, ni washiriki wane tu ndio
wanaoweza kutunukiwa zawadi. Hata hivyo, ni matumaini yangu kwamba hao washiriki
wengine hawatavunjika moyo, bali wataendelea kushiriki katika mashindano yafuatayo,
na kwamba baadhi yao watafarijika kwa maandishi yao kuchapishwa vitabu pia.
Yanastahili.
Mukoma Wa Ngugi, mwanzilishi-mwenzi wa
tuzo hii alisema, “Kiwango cha msaada tuliopokea kinadhihirisha kuwa kuna
uhitaji, na pia uwanja mpana, wa kuandika kwa lugha za Kiafrika; na kuwa
utamaduni wa Kiafrika wafasihi unaweza kustawi katika lugha za Kiafrika, na
kwamba lugha za Kiafrika zinaweza kukuzwa kupitia ufadhili kutoka Afrika
kwenyewe.”
LizzyAttree, mwanzilishi-mwenzi
mwengine wa tuzo hii alisema, “Tunawashukuru wote walioleta miswada yao katika
shindano hili, na tunatarajia kuwa tuzo ya mwaka huu itawahimiza waandishi
zaidi kushiriki katika shindano la mwaka ujao.”
MashartiyaTuzo:
1.Tuzo itatolewa kwa muswada bora
ambao bado haujachapishwa, au kwa kitabu kilichochapishwa miaka miwili kabla ya
mwaka wa tuzo, katika tanzu za riwaya, tamthilia, ushairi, wasifu, na riwaya za
michoro. Jumla ya dola za Marekani 15,000 zitatolewa zawadi kama ifuatavyo:
Zawadi ya Kwanza ya Riwaya - $5,000
Zawadi ya Kwanza yaUshairi - $5,000
Zawadi ya Pili katika utanzu wowote
- $3,000
Zawadi yaTatu katika utanzu wowote -
$2,000
2. Kitabu au muswada utakaoshinda
utachapishwa kwa Kiswahili na shirika la uchapishaji la East African
Educational Publishers; na diwani bora ya mashairi itatafsiriwa na kuchapishwa
na Africa Poetry Book Fund.
3. Sherehe ya kuwatuza washindi
wanne, itakayohudhuriwa na washindi wenyewe, itakuwa Kenya. Washindi hao
wataalikwa Chuo Kikuu cha Cornell, watakako kuwa kwa wiki moja; kisha wiki moja
nyingine watakuwa katika asasi shiriki (ya Marekani amaAfrika) mwaka 2016.
Shindano la mwaka 2016:
Washiriki wanaombwa kupeleka miswada
ambayo haijachapishwa, au vitabu (riwaya, tamthilia, ushairi, wasifu, au riwaya
za michoro), vilivyo chapishwa kwa Kiswahili miaka miwili kabla ya mwaka wa
tuzo, kwa: kiswahiliprize@cornell.edu
kabla ya Machi 31, 2016. Miswada ya
maandishi yanathari isipungue maneno 50,000; na ya ushairi isipungue kurasa 60.
Waamuzi:
Waamuzi watabadilishwa kila mwaka na
kuchaguliwa na wadhaminiwaTuzo.
TareheMuhimu:
Tarehe ya mwisho ya kupeleka miswada
au vitabu ni Machi 31, 2016. Orodha ya kwanza itatolewa Julai 2016, na washindi
watatangazwa Oktoba 2016.
KwaWahariri:
Tuzo ya Kiswahili ya Mabati Cornell ya Fasihiya Kiafrika ilianzishwa na Prof. Mukoma Wa
Ngugina Dk. Lizzy Attree mwaka wa 2014 ili kuendeleza uandishi bora kwa lugha
za Kiafrika na kuhimiza tafsiri kutoka lugha za Kiafrika kwa lugha nyingine,
pia baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe.
Tuzo ya Mabati-Cornell:
Kwa kiasi kikubwa, tuzo hii
inadhaminiwa na Mabati Rolling Mills of Kenya (sehemu ya Kampuni ya Safal),
Ofisi ya Makamu wa Mkuu wa Maswala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Cornell,
Idara ya Masomo na Utafiti ya Afrikana
Mabati Rolling Mills:
Mabati ni sehemu ya Kampuni ya
Safal, inayotengeneza mabati katika nchi 11 za Mashariki ya Afrika na Kusini
mwa Afrika.
Ofisi ya Makamu wa Mkuu wa Maswala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Cornell inatoa
mwongozo na kusaidia katika kusimamia juhudi za kuzidisha shughuli za kimataifa
Cornell. Lengo lake ni kushirikiana na shule, vyuo na vituo ili kuendeleza na
kutekeleza mipango inayohusiana na shughuli za kimataifa za Chuo Kikuuhiki.
Ofisi hii itaisaidia Halmashauri mpya ya Kimataifa, ambayo mwenyekiti wake ni
Makamu wa Mkuu.
Idara ya Masomo na Utafiti ya Afrikana ni Idara ya Masomo na Utafiti ya
Afrikana, mazingira ya kielimu, ya
kitamaduni na ya kijamii kwenye Chuo Kikuu cha Cornell, Ithaca.
East African Educational Publisher (EAEP) ni shirika moja wapo kuu la
wachapishaji. EAEP linajitahidi kuyahusisha maadili yanayoonekana kama kwamba
yanakinzana; yaani kuchapisha kazi za kiwango cha juu zinazogusia maswala ya kijamii,
ya kitamaduni na ya kiuchumi, na wakati huo huo kufaulu kufanya biashara iliyotayari
kukabiliana na hali halisi na misukosuko ya zama za kiteknolojia.
Africa Poetry Book Fund inaimarisha na kuendeleza uchapishaji wa sanaa za kishairi kupitia
vitabu vyake, mashindano, warsha na semina pamoja na kushirikiana na wachapishaji,
matamasha, mawakala, vyuo, vyuo vikuu, makongamano na vikundi vingine vinavyohusika
na ushairi Afrika.
Bodi ya Wadhamini:Abdilatif Abdalla (Mwenyekiti), Mukomawa Ngugi, LizzyAttree,
Happiness Bulugu, Walter Bgoya, Henry Chakava, Chege Githiora, Carole Boyce
Davies, Rajeev Shah, Ngugi Wa Thiong’o – na wengine watakaotangazwa baadaye.
Twitter: @KiswahiliPrize
KwaMawasiliano:
DrLizzyAttree, kiswahiliprize@cornell.edu
0 comments:
Post a Comment