November 19, 2015


wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemthibitisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania.
Jina hilo liliwasilishwa na bungeni na Rais wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli baada ya kumteua kushika wadhifa huo.
Kassimu Majaliwa ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa kupitia CCM jimbo la Ruanga alishawahi kuwa Naibu Waziri wa Tamisem.
majaliwa wamempitisha kwa kura 258 za ndio sawa na asilimia 73.5 na kura 91 zilikuwa za habana. 
Akizungumza baada ya kutangazwa amemshukuru Dkt Magufuli kwa kumuamini kushika nyadhifa hiyo kubwa kwa serikali.
Amewahakikisha wabunge hao kufanya kazi kwa pamoja na watu wote bila ya kujali itikadi za kisiasa katika kuwatukumia wananchi katika kusukuma maendeleo ya watanzania. 
Badhi ya wabunge waliohojiwa wamemsifia kiongozi huyo kwa utendaji bora na wanaamini ataweza kuwa chachu ya kusimamia serikali kwa ufanisi zaidi.  
Majaliwa aliezaliwa Disemba 22 1960 anatarajiwa kuapishwa kesho huko ikulu ndogo ya Chamwino Dodoma kuwa Waziri Mkuu wa 11 wa  Tanzania 2015-2020.

0 comments:

Post a Comment