December 16, 2015

Meli ya royal express imepata hitilafu ya moto kenye chumba cha Injini ikiwa safarini kuelekea kisiwani pemba na kusababisha taharuki kwa abiria waliokuwa wakisafiri na meli hiyo.
Katika meli hiyo iliyopata hitilafu hiyo wakati ikikaribia kisiwa cha Matumbilini karibu na gati ya Mkoani ilikuwa na abiria 300 wakubwa na watoto 67 na  wote wapo salama.
Chanzo moto huo uliochukuwa dakika 15 inadaiwa umesababishwa  baada ya kupasuka paipu ya Hydraulic ya mashine ya upande wa kulia .
Wafanyakazi Waliomba msaada Bandarini Mkoani na pia msaada mkubwa ulitolewa na meli ya Serengeti, iliyokuwa inatokea Mkoani kuja Unguja muda huo wa tukio na kufanikiwa kuzima moto na pia kifungasha meli ya Royal hadi bandarini Mkoani.
Abiria wote wameteremka salama isipokuwa mmoja yao anaeitwa Othman Ali Mussa amepata majeraha baada ya kujaribu kuvunja  dirisha la kioo kwa kutumia mguu wake.
Mv Royal I imeondoka bandari ya Malindi asubuhi saa 1.04 ikiwa pia na abaria hao na mabaharia 11.
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba na viongozi mbali mbali walifika bandarini Mkoani kuisubiri boti hiyo iliyokuwa inavutwa na meli hiyo ya Serengeti na tagi za bandarini  na boti ya majeshi ambazo zilikwenda kwa uokozi.
Akizungumzia chanzo cha tukio hilo Kepteni wa boti ya Royal Express I Mohamed Ali amewambia wananchi waondoshe hofu juu ya tukio hilo, kwani mashine za boti hazina matatizo na wala hazihusiani na ajali jiyo.
Baadhi ya abiria waliokuwemo katika boti hiyo wamesema walisikia kitu kimepasuka na kuona moto na moshi nyuma ya boti hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid Abdalla amevishukuru vyombo vyote vilivyoshiriki katika uokozi huo kwa juhudi walizochukuwa hadi meli hiyo inafika bandarini.
Abiria wote wameteremka salama isipokuwa mmoja yao anaeitwa Othman Ali Mussa amepata majeraha baada ya kujaribu kuvunja  dirisha la kioo kwa kutumia mguu wake.   





0 comments:

Post a Comment