November 19, 2015


Serikali ya Zanzibar imewataka wananchi kufuata taratibu na maelekezo ya kujikinga na athari za mvua pamoja na kutafuta maeneo mbadala ya kuishi kwa muda mpaka kumalizika kwa mvua hizo.
Waziri wa nchi afisi ya Makamu wa pili wa Rais Mohammd Aboud Mohammed amesema taratibu ni pamoja na wote wanaoishi karibu na mabonde kuhama maeneo hayo kwani kutawasaidia kujiepusha na athari za majanga yanayoweza kujitokeza.
Ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi msaada wa fedha kwa familia 11 kati ya 44 zilizoathirika zaidi na mvua hizo katika maeneo ya shehia ya mwanayanya na mtoni kidato wilaya ya Magharibi “A”.
Tumetoa msaada huo ili kuwasaidia wananchi hawa baada ya tathmini ya awali….. lakini serikali  inaendelea kufanya tathmini zaidi kwa wananchi wote waliopata maafa haya ya mvua.


0 comments:

Post a Comment