April 18, 2014


Rais Jakaya Kikwete amesema cha baadhi ya Watanzania kuwatukana, na kuwakejeli viongozi waanzilishi wa Taifa la Tanzania Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume ni utovu wa nidhamu.

Amesema kuwa viongozi hao wawili wameifanyia Tanzania mambo mengi ya kihistoria hivyo Watanzania wanao wajibu wa kuendelea kuwaenzi na kuwaheshimu.
Rais Kikwete ametoa msimamo huo wakati akielezea kuhusu matusi, kejeli, dhihaki za baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba linaloendela mjini Dodoma juu ya waasisi hao wa Tanganyika na Zanzibar walioamua kuungana na kuanzisha taifa la  Tanzania.    

Rais Kikwete wakati akitoa taarifa hiyo Viongozi wa wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika bunge hilo maalum wasema hawatarejea tena katika Bungeni na badala yake wanaenda kuwaelezea wananchi kilichotokea baada ya kutoka bungeni kwa madai ya kauli za  mabishano na matusi kwa baadhi ya wabunge wa kambi kuu.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali uongozi  UKAWA wanatarjiwa kufanya mkutano mjini Zanzibar mjini Zanzibar  mwisho mwa juma hili.

 




0 comments:

Post a Comment