Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema,
anaimani kubwa kwamba ushirikiano uliopo baina
ya serikali mbalimbali barani Afrika, mashirika ya kimataifa,
makampuni binafsi na kila mtu katika nafasi yake, hapana shaka
ugonjwa wa malaria unaweza kumalizwa kabisa.
Mhe. Kikwete ameonyesha matumaini hayo jana( alhamisi)
wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa
jitihada za kuutokomeza ugonjwa wa malaria (Malaria
No More) zilizoanzishwa na Bw. Ray Chambers akishirikiana
na Bw. Peter Chernin.
Katika hafla hiyo na ambayo mshereheshaji alikuwa
Bw. Wolf Blitzer mtangazaji maarufu wa Televisheni ya Kimataifa ya
CNN kupitia kipindi chake cha situation Room, Rais mstaafu
alitunukiwa tuzo ijulikanayo kama White House Summit
Awards ikiwa ni kutambua uongozi wake, kujitoa kwake
na kubwa zaidi kusimamia uanzishwaji wa muungano wa
viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria (ALMA) muungano ambao hadi sasa
una viongozi 49.Wengine waliotunukiwa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na
Sumitomo Chemical.
Akijibu swali la nini anadhani kumechangia katika kupunguza
idadi ya vifo
vitokanavyo na ugonjwa wa malaria.
Rais mstaafu amesema, zipo sababu kadhaa,
lakini kubwa ni utashi wa kisiasa wa kusimamia na kuongoza
mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Akawaeleza wageni zaidi ya 250 walioalikwa wakiwa ni wawakilishi wa
makapuni na mashirika mbalimbali yanayochongia juhudi za kuukabili
ugonjwa wa malaria. Kwamba, Upatikanaji na usambazani wa dawa sahihi
za kutibu ugonjwa
wa malaria, utengenezaji, usambazaji na
matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu na unyunyiziaji wa dawa za kuuwa mazalia
ya mbu ni mambo ya msingi ambayo yamechangia
katika kupunguza vifi vya watoto chini ya miaka mitano.
“mchanganyiko wa mambo hayo matatu umesaidia sana kupunguza idadi
ya watoto wanaofariki kwa malaria, lakini pia matumizi
ya vyandarua vyenye viatilifu ambapo zaidi ya
vyandarua milioni 24.2 vimesambazwa, kumechangia
wanafunzi kuendelea na masomo yao bila kukatishwa mara kwa mara sababu ya
malaria, halikadhalia nguvu kazi imeimarika”. akasisitiza Rais Kikwete na
kushangiliwa na wageni waalikwa.
Mhe. Rais Mstaafu katika mkutano na Bodi mpya
ya Malaria no More muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya miaka 10 ya Malaria No More. |
:Mwandishi Maalum, New York
0 comments:
Post a Comment