April 08, 2016


Shirika la umeme Zanzibar  ZECO  linakusudia kuanza kazi ya ubadilishaji wa miundo mbinu ya usambazaji wa umeme vijijini ili kuimarisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi
Kazi zitakzofanyika ni uwekaji wa nguzo, nyanya na taransforma mpya katika Mkoa yaKusini na Kaskazini Unguja na Pemba unatarajiwa kuanza April 25, 2016.
Meneja sera na mipango wa ZECO Abdala Haji Steni amewaambia waandishi wa habari mjini Zanzibar kuwa Kazi hiyo inatekelezwa kupitia mradi wa wa miaka minne wa kuliwezesha kiufundi shirika hilo unaofadhiliwa na Serikali ya Norway utahusisha unaogaharimu Shilingi bilioni 23. 4.
Amesema kutokana na kazi hiyo huduma ya umeme katika maeneo hayo italazimika kuzimwa kwa siku 3 kila wiki kuanzia saa 12 asubuhi hadi 1 jioni.
Steni amesema kwa kuwa nishati ya umeme ni kichocheo cha maendeleo amewaomba wananchi na wawekezaji wa sekta ya utalii ambao wapo wengi katika maeneo hayo kuwa wastahmilivu kwa vile kinachofanyika kuondosha usumbufu wa kukatika ovyo umeme kutokana na uchakavu wa vifaa na miundo mbinu yake na kukwamisha maendeleo  ya taifa na jamii.
Kwa upande wake afisa uhusiano wa ZECO Salum Abdalla amesema kwa sasa tatizo kubwa linalowasumbua ni wizi wa nyaya na vifaa vya umeme hasa vya shaba mbali na juhudi kadhaa wanazozichukuwa hivyo amewaomba wananchi kusaidia katika ulinzi wa miundombinu ya umeme kwa vile wanaohusika na vitendo hivyo wamo katika jamii zao.

Meneja sera na mipango wa ZECO Abdala Haji Steni
Afisa uhusiano wa ZECO Salum Abdalla


0 comments:

Post a Comment