Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna Kilango Malecella, kwa kubaini kuwa alimwambia
uongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa.
Rais Magufuli amesema hakuamini kuna mkoa uliokuwa hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi
ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuwepo wafanyakazi hewa 45
mkoani Shinyanya.
Rais pia ametengua uteuzi
wa Katibu Tawala wa Mkoa huo Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu
wa Mkoa.
Akizungumza baada ya kupokea
Ripoti ya TAKUKURU toka kwa Mkurugenzi wake Mkuu Valentino Mlowola,
Rais Magufuli amesema kasikitishwa sana na kauli ya Mama Malecela ambaye
bila shaka alikuwa amepata ushauri mbaya toka kwa watendaji wake.
Rais Magufuli amesema pia hadi jana jumla ya wafanyakazi hewa zaidi ya 5,507 wamebainika nchi
nzima, wengi wao wakitoka katika halmashauri.
Katika hatua nyengine
ametoa siku 15 kwa wakurugenzi wa halmashauri
kuwatotoe katika Orodha ya Malipo ya Mshahara (Pay Roll) wafanyakazi hewa wote
katika halmashauri zote nchini, na kuwataka wakuu wa Mikoa hao wasimamie zoezi
hilo kwa ukamilifu.
0 comments:
Post a Comment