Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano
na Usafirishaji Mhe Balozi Ali Karume amesema suala la umoja na ushirikiano ni
muhinu katika utendaji wa kazi ili kuleta ufanisi bora kazini.
Mhe Waziri amesema hayo
alipokutana na uongozi wa Wizara hiyo ikiwa ni siku yake ya mwanzo kuripoti
kazini tokea aapishwe wadhifa huo.
Amesema nidham ya kazi ni
kitu kikubwa sana kazini kwani huleta heshima, mshikamano kwa wakubwa na wadogo.
Katika mazungumzo yake na wakuu wa Wizara hiyo waziri karume amewaomba wakuu hao kuwa na utaratibu mzuri wa fursa za mahitaji ya fedha na kuzijngea hoja madhubuti serikalini na sehemu nyengine za mahitaji na kuonesha mrajesho sahihi.
Hata hivyo amesema
upatikanaji wa fedha na matumizi yaende sambamba na lengo lililokusudiwa na sio
kwenda kinyume na lengo husika.
Mh karume amefahamisha
kuwa lengo la Rais kuanzisha Wizara hiyo ni kuwepo uhusiano mkubwa kwa taasisi zake na taasisi
zilizokuwa katika Wizara kama hiyo ya Tanzania Bara ili kurahisisha kuwa na
ushirikiano mkubwa kwa kutatua kero zinazozikabili taasisi hizo.
Aidha amesema Wizara hiyo
kwa sasa itajikita zaidi na masuala ya ukarabati na utunzaji wa nyumba na
barabara ili Zanzibar iwe na Mazingira mazuri kama yalivyo mataifa mengine.
Waziri karume ameomba ushirikiano
na kusaidiwa kazi na wakuu hao ili wawezee kufikia lengo lililokusudiwa.
0 comments:
Post a Comment