Leo April 7, 2016 ni siku ya kumbukumbu ya
miaka 44 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume aliefariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa
risasi.
Mzee Karume alizaliwa mwaka 1905 aliongoza Zanzibar
baada ya Mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Visiwa vya Zanzibar
hadi mwanzoni mwa mwaka 1964.
Miezi mitatu baadae Zanzibar iliungana na Tanganyika
iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere na kuanzisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mzee Karume alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Tanzania.
TAZAMA MAKALA FUPI YA MZEE KARUME
0 comments:
Post a Comment