Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar imeaandaa
mpango maalum wa kuhamasisha jamii umuhimu wa upandaji wa miche ya
misitu, matunda na mikarafuu ili zanzibar iweze kuzalisha mazao kwa wingi.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Afan Othman
Maalim amesema mpango huo unalenga pia katika kukabiliana na uharibifu wa
mazingira pamoja na kukabiliana na
mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
upandaji wa miti kwa msimu wa mvua za masika amesema utafiti unaonesha jumla ya
maeneo 47 yameathirika na uharibifu huo hivyo ni vyema jamii kuendeleza kupanda
miti kwa wingi ili kujinusuru na athari hizo.
Katibu mkuu Maalim amesema upandaji wa miti
kitaifa kwa mwaka huu utafanyika katika maeneo mbalimbali ya zanzibar ikiwemo
yale yaliothirika zaidi ili kuyarejeshea haiba yake.
Amefahamisha kuwa katika mwaka huu wa 2016 Serikali kupitia
Idara ya misitu na Maliasili zisizorejesheka inakusudia kugawa miche zaidi ya
milioni moja na kali nne kwa wananchi mwaka
huu.
ametoa wito kwa wakulima kuihudumia miche
watakayopanda ya mikarafuu, matunda na misitu na kuhakikisha kuwa mashamba yao
yanakuwa safi kwa ajili ya upandaji.
0 comments:
Post a Comment