SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua
kuanzisha utaratibu wa kutumia njia ya upande mmoja kubwa ya kuingia Mji
Mkongwe kuanzia tarehe nane mwezi huu ili kupunguza usumbufu unaowapata wageni
na watumiaji wengine wa Mji huo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mamlaka ya Mji Mkongwe Forodhani, Mkurugenzi Mkuu Issa Saidi Makarani amesema uwamuzi huo umefikiwa kutokana na ongezeko kubwa la vyombo vya moto linalohatarisha usalama wa mji huo ambao ni urithi wa kimataifa.
Amesema mji wa Zanzibar umekuwa ukipokea watalii na wageni wengi na wakati wa matembezi yao wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa kutokana na kuongezeka vyombo hivyo.

Ameongeza kuwa ongezeko hilo la magari pia
limepelekea athari kubwa kwenye majengo kutokana na mtikisiko mkubwa wa magari
yenye uzito mkubwa na kubomoa baadhi ya majengo ya mji.
“Watumiaji wa Mji huu na wanaofika kila siku
kwa shughuli zao za kimaisha wanapata usumbufu na kubwa zaidi wingi wa vyombo
hivyo tayari vimesababisha athari ya baadhi ya majengo,” alisisitiza Mkurugenzi
Makarani.
Amesema njia kubwa ya ndani ya kuingilia Mji
Mkongwe itaanzia Vuga kupitia Afrika House , Hoteli ya Serena , Wizara ya Ardhi
, Makaazi, Maji na Nishati , Benki ya NBC , Jengo La zamani la Watoto Forodhani
, njia ya Mizingani hadi kuishia lango kuu la kuingia bandarini Malindi.
Amezitaja njia zitakazofungwa kuanzia tarehe
nane kuwa ni ile inayoanzia jengo la Wizara ya zamani ya Mawasiliano na
Uchukuzi kupitia Kiponda na kumalizikia Darajani, njia inayoingia Mkunazini na
kumalizikia Skuli ya Sunni Madrassa na njia inyozunguka nyuma ya jengo la
sinema ya zamani Majestic.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi
Mkadam Khamis amesaema lengo la kuweka zoezi hilo ni kuweka usalama kwa wenye
magari na wanaokwenda kwa miguu.
Amewaomba wananchi kuunga mkono zoezi hilo
ambalo litaweka mji Mkongwe katika hadhi na ubora wake uliopelekea kuwa
miongoni mwa Miji ya Urithi wa kimataifa duniani.
Mkurugenzi wa Baraza la Manispaaa Aboud Hassan
Serenge amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya Mji Mkongwe kubadilika na
kuanzisha utamaduni wa kuimarisha suala la usafi.
Maelezo Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment