Wakati Chama cha wananchi CUF ambacho ni chama kikuu
cha Upinzani visiwani Zanzibar kikiwa kimesusia uchaguzi wa marudio ambao
unafanyika Marchi 20 ya mwaka huu,Baraza la Waislam (BAKWATA)
limesema marudio ya uchaguzi huo ndo njia ya kipee ya kurudisha amani
visiwani humo..
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Jijini Dar es Salaam,
Sheikh Mkuu mkoani hapa,heikh alhadj Mussa Salum amesema Bakwata
wanaunga mkono Tangazo la ZEC la kurudiwa kwa uchaguzi huu.
“Uchaguzi huu wa marudio
kwetu Bakwata tunaona ndio njia ya kipekee ya kukiweka kisiwa cha Zanzibar kuwa
sehemu ya Amani na utulivu,natumia nafasi hii kuwaomba chama cha CUF kushiriki
uchaguzi huu” Amesema
Sheikh Salum.
Sheikh Salum ameongeza kwa kusema kuwa hata kiongozi
wa jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmad amemwandikia
barua na kumweleza kuwa kurudiwa kwa uchaguzi kutasaidia kurudisha Amani
visiwani humo.
Katika hatua nyingine, Baraza hilo limeipongeza
serikali ya awamu ya tano kwa jitihada mbalimbali inazofanya za kuimarisha
nidhamu, kubana matumizi na kukuza uchumi.
"Pia tunaipongeza serikali
ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mh. John Magufuli, kutokana na hatua mbali
mbali inazozichukua zenye lengo la kuimarisha nidhamu hasa kwa watumishi wa
umma, hatua mabazo zimeanza kuleta tija kubwa ka taifa letu kama wote hivi leo
tunavyoweza kushuhudia jinsi pato la serikali likongezeka mwezi hadi mwezi”, alisema Sheikh alhadj Mussa
Salum na kuongeza;
“Aidha tunaipongeza kwa dhamira
yake ya kubana na kupunguza matumizi ya serikali, na badala yake kuelekeza
fedha kwenye huduma za jamii na watanzania tumeshaanza kunufaika na huduma hizo
kama vile suala la elimu bure."
0 comments:
Post a Comment