Matumizi ya dollar za kimarekani yamekuwa
yakiongezeka siku hadi siku, hii imepelekea kuongezeka kwa thamani ya pesa hiyo
kulinganisha na thamani ya pesa nyingine.
Miaka ya hivi karibuni kulikuwa na mkanganyiko
na mikakati ya kurudisha thamani ya shilingi ya Kitanzania, lakini suala hili
imekuwa si tatizo kwa nchi ya Tanzania pekee bali ni kwa
nchi nyingi barani Afrika. hata hivyo JovagoTanzania imejaribu
kutathmini thamani ya dola moja ya kimarekani na nchi kumi barani Africa ili
kuitambulisha thamani yake ukiwa nje ya nchi.
Dolla moja imeonekana inathamani ya kipekee na
kugundulika kuwa kwa Tanzania inaweza kusaidia kununulia muda wa maongezi na
Vitu vingine vidogo vidogo, lakini kwa baadhi ya nchi nyingine kama Nigeria
unaweza kupata hadi lita mbili za mafuta ya petroli.
Hata hivyo thamani ya pesa hutofautiana kati ya
nchi na nchi, baadhi ya pesa zenye nguvu duniani ni pamoja na Kuwait dinar,Bahrain dinar,Oman rial, latvia
lats, Uk Pound na Dola ya Kimarekani. Swali la kujiuliza pesa ya Tanzania ipo
katika kiwango kipi!, ni kwa nini shilingi ya Kitanzania inashuka!, je kuna
uwezekano wowote shilingi yetu ikapanda!
0 comments:
Post a Comment