Zaidi ya shilingi milioni mia
moja zimekusanywa na Idara ya Mazao ya baharini Zanzibar kufuatia kuuzwa kwa
mazao ya baharini ne ya nchi katika kipindi cha mwaka jana 2015
Makusanyo hayo ni ongozeko la
shilingi milioni 69 zilizokusanywa
katika mwaka 2014 kwa bidhaa za
mwani, dagaa, kamba, majongoo na kaa .
Mkurugenzi wa idara hiyo Mohamed
Soud Mohamed amesema ongezeko hilo linatokana na mwamko wa wananchi
kujishughulisha na uvuvi wa kibiashara kufuatia zingatia taaluma zinazotolewa
katika kukabiliana na soko la usindani kimataifa.
Hata hivyo amesema kuna upungufu
wa usafirishaji nje ya nchi pweza na ngisi
kutokana na kuimarika soko la ndani hasa kwa kukua kwa sekta ya utalii
nchini.
Mkurugenzi
Mohamed ameyataja mazao mengine ya baharini yanaongoza katika kuingiza fedha ni
dagaa liokusanya shilingi millioni kumi na tisa na shillingi miilioni thamanini
kwa zao la mwani.
0 comments:
Post a Comment