Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali
imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha
wananchi kiuchumi.
“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10
tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa
mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za
kiuchumi zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,”
amesema.
Waziri Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na
sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya
wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara,
utalii, madini, viwanda na usafirishaji.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne,
Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau
wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha
kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe.
Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe.
Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa
Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua
mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na
Walemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo
ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake na imeanza kuweka miundombinu ya
kuvutia wawekezaji.
Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa amesema katika dunia ya sasa
imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au
kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa
kuwaunganisha na masoko.
0 comments:
Post a Comment