January 18, 2016


HALI YA KIPINDUPINDU ZANZIBAR
Tokea mwezi wa Septemba 2015 Zanzibar imekua ikikabiliwa na mripuko wa Kipindupindu ambapo mgonjwa wa mwanzo kabisa wa maradhi haya aliripotiwa tarehe 19/09/2015 katika hospitali ya Mnazi Mmoja kwa Unguja na terehe 2/11/2015 katika hospitali ya Wete kwa Pemba.
Hadi kufikia 12 Januari 2016, jumla ya wagonjwa 1204 wameshalazwa katika vituo 13 vilivyokwishafunguliwa Unguja na Pemba. Vituo hivyo ni Chumbuni, Uzi, Muungoni na  Uroa kwa Unguja; na Mkoani Nursery, Kojani, Mjini Kiuyu, Makangale, Vitongoji, Jadida, Micheweni, Maziwa Ngombe, Kiuyu Mbuyuni. Vituo vya Uzi na Muyuni kwa Unguja na Mkoani Nursery, Kojani, Mjini Kiuyu na Makangale kwa Pemba vimeshafungwa baada ya kukosa wagonjwa kwa zaidi ya wiki 3.
Zaidi ya asilimia 90 ya wagonjwa wote wa Unguja wa metokea wilaya za mjini na Maghribi A na B; na asilimia 90 ya Wagonjwa wa Pemba wametokea Wilaya za Wete na Micheweni
Jadweli hapa chini inaonyesha idadi ya wagonjwa wa Kipindupindu na Wilaya walizotoka Unguja na Pemba:
WILAYA
IDADI YA WAGONJWA
%
Unguja
MAHARIBI A&B
341
64.6
MJINI
128
24.5
KATI
28
5.4
KASKAZINI B
17
3.3
KASKAZINI A
9
1.7
KUSINI
3
0.6
Total Unguja
526
43.7
Pemba
WETE
367
54.1
MICHEWENI
246
36.3
CHAKE CHAKE
61
9.0
MKOANI
4
0.6
Jumla Pemba
678
56.3
JUMLA ZANZIBAR
1204
100.0
 WITO KWA WANANCHI
Ni muhimu kuelewa kwamba, Kinpindupindu bado kipo Zanzibar na maambukizi yanaendelea kuongezeka siku hadi siku. Hali hii imekua ikiathiri sana afya na shughuli za kimaisha katika Jamii yetu. Ili kuepukana na maradhi haya kila mwananchi hana kufuata maelekezo ya kiafya na kuzingatia yafuatayo:
1.Kufukuzia kituo cha Afya au kituo cha cha matibabu ya Kipindupindu mara tu uonapo dalili za kuhara na kutapika huku ukinywa maji kwa wingi
2.Kuhakikisha tunakunywa maji yaliyo safi na salama muda wote kwa kuyachemsha au kutia dawa ya kusafisha maji (water-guard).
3.Kuosha mikono kwa maji yenye kutiririka na sabuni baada ya kutoka msalani, baada ya kumsafisha motto aliyejisaidia, kabla ya kula na wakati wa kutayarisha chakula.
4.Kuwa waangalifu na vyakula tunavyo kula kwa kutokula vyakula visivyotayarishwa katika mazingira safi na salama.Pendelea kula chakula kikiwa na uvuguvugu na epuka viporo.
5. Kuosha vyema Matunda na mboga za majani kwa kwa maji ya mtiririko kabla ya kula.
6.Tutumie choo kwa usahihi muda wote tunapotaka kujisaidia.
7.Tuepuke kutupa ovyo kinyesi matapishi na Penpas kunakopelekea kusambaa kwa maradhi haya
8.Tusafishe majaa, mitaro na maeneo mengine ya nayotuzunguka ili kuepuka inzi na kusambaa kwa maradhi kutoka mtu mmoja kwenda mwengine
9.Mgonjwa yeyote anayeshukiwa kufariki kwa kuharisha na kutapika ni lazima azikwe chini ya uangalizi maalum wa wataalam waWizara ya Afya

KUMBUKA: KIPINDUPINDU KINAZUILIKA, CHUKUA TAHADHARI ILI KUJIKINGA KWANI KINGA NI BORA NA RAHISI KULIKO TIBA.
ZANZIBAR BILA KIPINDUPINDU INAWEZEKANA

0 comments:

Post a Comment