Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imepiga
marufuku kitendo cha baadhi ya skuli za sekondari kuawatoza wanafunzi michango
ya fedha tofauti na kiwango kilichoruhusiwa na serikali.
Katibu mkuu wizara hiyo Khadija Bakari Juma amesema
kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi kuwa baadhi ya
skuli inawalazimiasha wanafunzi kuchangia kiwango kikubwa cha fedha kinyume na tamko la serikali la mwaka 1999.
amefahamisha tamko hilo limelekeza viwango vya
uchangiaji kwa mwanafunzi ni shilingi 5000 kwa darasa la tisa
na kumi, kidato cha tatu na cha nne ni shilingi 7500 na kidato cha tano
na sita wanatakiwa kulipa shilingi 10000 tu.
Akizungumza katika kikao cha walimu wakuu na
watendaji wa Wizara ya elimu na mafunzo ya amali amewataka walimu kulisimamia
tamko hilo kwa ajili ya maendeleo ya wanafunzi kwani bado linaendelea
kutumika.
Katibu Khadija ameomba walimu hao kuwajibika katika kazi zao na
kuhakikisha wanamaliza mihutasari ya masomo na kuacha kuwafundisha wanafunzi
kikamilifu ili kuongeza ufaulu.
Kwa upande wao
walimu hao wakuu wameiomba wizara ya elimu kufanikisha
upatikanaji wa vifaa vya kufundishia katika skuli pamoja na kuharakisha uungwaji wa huduma za
maji na umeme ili kupunguza viwango hivyo vya uchangiaji kwa wazazi.
0 comments:
Post a Comment