January 19, 2016

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesema licha Vyuo Vikuu Nchini  kuendelea kutoa taaluma kwa vijana bado vina wajibu na jukumu  kubwa la kuhakikisha wasomi wake wanatumia vipaji vyao katika kufanya  tafiti  kwenye maeneo mbali mbali.
Amesema tafiti hizo zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwa wasomi  wachanga wanaoanza kupata taaluma kwenye  Vyuo hivyo sambamba na kuliwezesha Taifa kupiga hatua za haraka za Maendeleo.
Dr. Ali Moh’d Shein ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 15 ya Wahitimu 686 wa Satashahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha  Elimu cha  Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al - Sumait kiliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Amesema kuimarika kwa  eneo la utafiti pia kutatoa fursa kwa wananchi mbali ya kupata elimu katika kiwango cha juu lakini pia watapata mbinu na maarifa ya kukabiliana na changamoto zilizowakabili maisha yao ya kila siku.
Rais wa Zanzibar alisema mchango mkubwa unaotolewa na  Vyuo vikuu hapa Nchini hasa vile   Binafsi umesaidia ongezeko la Walimu wa skuli mbali mbali za Sekondari hapa Visiwani.
“ Vyuo hivi vikuu tayari vimeshazalisha idadi kubwa ya wahitimu ambao kwa sasa wanatoa taaluma katika masomo tofauti kwenye skuli mbali mbali hapa nchini ”. amesema Dr. Shein.
Ameushauri Uongozi wa Vyuo vikuu vya Zanzibar kuendelea kushirikiana pamoja katika kubadilishana uzoefu wa Kitaaluma kwa lengo la kuwajengea mazingira bora Walimu pamoja na Wanafunzi wa vyuo vyao.
Mapema, Mkuu wa Baraza la Chuo hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany, amesema miongoni mwa malengo ya chuo hicho, ni kudumisha umoja wa vyuo vya hapa nchini na nje ya Tanzania.

Balozi Seif Ali Iddi akipokea zawadi maalum kutoka
kwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho
Dr. Abdulrahman Al – Muhailan kwenye mahafali
ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.





0 comments:

Post a Comment