Tishio la ajira za Wafanyakazi 350 wa Kiwanda
cha Sukari Mahonda zinaendelea kuwa hatarini kufuatia kuendelea kwa hujuma za kuyachoma moto mashamba ya miwa ya kiwanda sukari cha Mahonda
Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Hii ni kufuatia Kiasi ya Eka 50 za Miwa
iliyopevuka kuteketezwa kwa moto na kusababishia
Kiwanda hicho hasara ya Tani 200 za Sukari na Lita 2,300 za Spititi zilizogharimu
zaidi ya shilingi Milioni 494 za Kitanzania.
Heka hizo zimechomwa na watu wasiojulikana ikiwa
ni siku tano tangu baada ya shamba hilo la
Miwa kuchomwa karbu heka 150 Tarehe 30 mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa
Kiwanda cha Sukari Mahonda hasara iliyopatikana kwa kiasi Eka 200 zilichomwa moto ni shilingi za
Kitanzania Bilioni 2,326,818,500/-.
Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari
Mahonda Tushar Mehta amesema kuendelea
kwa hujuma hizo Uongozi wa Kiwanda hicho kinaweza kufikiria kufuta ajira mpya
450 za Wafanyakazi baada ya kukamilika
matengenezo makubwa na kuanza tena uzalishaji wa sukari.
Amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kuangalia hasara ya moto uliotiwa katika shamba
hilo katika kipindi cha siku Tano baada ya tukio kama hilo la Tarehe 30 mwezi
uliopita.
Akitoa pole Uongozi wa Kiwanda hicho Balozi
Seif amesema hujuma hiyo ya makusudi haiitakii mema Zanzibar katika harakati
zake za kustawisha uchumi wake na amewasihi watu wenye tabia hiyo kuacha kwani inawavunja
moyo wawekezaji walioamua kuja kuwekeza miradi yao ya kiuchumi Zanzibar kwa
lengo la kuisaidia Serikali pamoja na Wananachi wake.
“ Haya
ni Mashamba ya Serikali yaliyotengwa maalum kwa shughuli za harakati za
Viwanda. Hivyo ndoto za baadhi ya Watu kufikiria kwamba hujuma zao
zitazaa matunda kwa kufanya wanavyotaka zinapaswa ziachwe mara moja ”. amesema
Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliufahaisha
Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kwamba Serikali Kuu inaangalia mpango
utakaowezesha Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusaidia ulinzi
kwenye Mashamba hayo ili kulinda hujuma zinazoonekana kushamiri siku hadi siku.
Hilo ni tukio la sita la hujuma za moto kwenye
mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda tokea kianze tena
uzalishaji wa sukari na Spiriti mapema mwaka uliopita wa 2015.
![]() |
Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda
Tushar Mehta akimueleza Balozi Seif hasara
iliyopatikana
kutokana na hujuma ya moto kwenye
mashamba ya Miwa la kiwanda cha
Sukari Mahonda,
|
0 comments:
Post a Comment