Wananchama wa chama cha wafanyakazi wa
huduma za Umma na Afya ZPHE wameiomba Chama cha wafanyakazi Zanzibar ZATU kufuatilia
juu ya baadhi ya wafanyakazi wa taasisi za umma kusita kuingiza nyongeza za
mishahara iliyoidhinishwa na Serikali.
Wamesema nyongeza hizo zimeshaingizwa kwa karibu miezi
sita sasa lakini wafanyakazi katika baadhi ya taasisi hawajaingiziwa nyongeza hiyo ya shilingi 25,000 hadi
sasa wakati wote ni wafanyakazi wanaotumikia Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Wakitoa michango yao katika mkutano wa kutoa taarifa
ya sherehe za wafanyakazi May day wameiomba ZATUC kufuatilia kasoro hiyo kwa vile kinaonesha kutokuwepo
haki na usawa kwa watendaji hao wa sekt ya umma.
Kwa upande mwengine wafanyakazi hao wameomba
kuangaliwa uwezekano wa kuongezwa kiinua mgongo kwa wafanyakazi wanaostahafu
kama wanavyopatiwa wanasiasa ili nao waishi maisha mazuri baada ya kustahafu.
Nae katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya
wafanyakazi Zanzibar ZATUC Khamis Mwinyi amesema watafuatilia tatizo hilo ili
kuona haki inatekelezwa.
Ameeleza kuwa maadhimisho ya May day mwaka huu
yameanza kwa shughuli za upandaji wa miti katika maeneo ya maruhubi na
zitaendelea kwa maonyesho ya taasisi mbali mbali yatakayofanyika katika viwanja vya amani.
0 comments:
Post a Comment