Wakaazi wa shehia za Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja wamesema vitendo vya rushwa vinachangia kukosa haki zao kwa kesi wanazozifikisha katika vyombo vya sheria.
Wamesema kuwa kwa sasa imekuwa na ugumu kwa wananchi wanyonge kupata haki yao katika vyombo hivyo.
Akizungumza katika mkutano wa elimu ya sheria kwa niaba ya wanashehia wenzake Ussi Suluhu Ussi amefahamisha kuwa kuna baadhi ya wananchi ardhi zao zimechukuliwa kinyume cha sheria lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa tangu kuwasilisha malalamiko yao.
Amesema katika kunusuru hilo wameishauri Serikali kufuatilia kwa makini utendaji kazi katika ngazi ya mahakama ili kuondoa udhaifu wa upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Mkurugenzi wa kituo cha huduma za sheria Harusi Miraji Mpatani amewataka wanajamii kuacha vitendo vitakosababisha kuwanyima haki zao ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima katika jamii.
Mkutano huo ni mwendelezo wa utoaji wa elimu ya sheria kwa wananchi katika mikoa ya Zanizbar iliyoandaliwa na kituo cha Huduma za Shehria na Shirika la kimataifa linaloshughulikia migogoro ya wananchi Search for Common Ground.
0 comments:
Post a Comment