April 29, 2014


Muonekano wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kilivyo hivi sasa.


Mshauri muelekezi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Dk. Hamza Hussein Sabri (alie simama) akitoa maelezo na changamoto wanazozipata Kiwandani hapo, kwa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la wawakilishi walipoenda kutembelea Kiwanda hapo.


Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la wawakilishi Hija Hassan Hija akizunguza na uongozi wa Kiwanda cha Sukari na viongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko katika kuangalia hatua ya uzalishaji Sukari Kiwandani hapo na changamoto wanazokabiliana nazo.


Afisa utumishi wa Kiwanda hicho Bw. Bashir Mohammed akionyesha kiroba cha kilo 50 za Sukari.


Mkurugenzi wa maendeleo ya viwanda Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Bw. Saleh Suleiman Hamad akiwaonyesha wajumbe wa Baraza la wawakilishi Sukari iliozalishwa kiwandani hapo ambayo bado haijaingia sokoni hadi sasa.

0 comments:

Post a Comment