Hospitali ya Mnazi mmoja inakabiliwa na
ukosefu wa sehemu ya kutoa matibabu ya magonjwa ya macho hali inayokwamisha
utoaji wa huduma hizo kwa ufanisi kwa wananchi.
Katibu wa hospitali hiyo Hassan Makame
Mcha amesema jengo walilokuwa wakitumia kutoa huduma hiyo limeshindikana
kuendelea kutumiwa licha ya kufanyiwa matengenezo mara mbili.
Amefahamisha kuwa wafadhili
wamejitokeza kulijenga upya jengo hilo ili kutoa tiba za macho kulingana na teknolojia
za kisasa lakini mamlaka ya Mji mkongwe imekataa ujenzi wowote ulio kinyume na
asili ya jengo hilo.
Katibu huyo ameiomba serikali kusaidia juhudi za
kufanikisha upatikanaji wa jengo la matibabu hayo katika hospitali ya mnazi
mmoja ili kuondosha usumbufu wa utoaji wa matibabu hayo uliopo sasa.
Akitoa
ufufanuzi kuhusu kusitisha ujenzi wa jengo hilo Mkurugenzi wa mamlaka ya
uhifadhi wa Mjimkongwe Issa Sariboko Makarani amethibitisha kuzuia ujenzi wa
jengo hilo kwa vile unaweza kupoteza hadhi ya miji ya kihistoria ya urithi wa
kimataifa.
0 comments:
Post a Comment