Wizara ya afya imetakiwa kutoridhia kuwa kuwepo majengo na
vifaa vya tiba kama ndio kigezo pekee cha mabadiliko ya sekta ya afya wakati hakuna
watendeji wa kutosha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed
Shein amesema mpango huo ni lazima uwende sambamba na kuimarisha huduma za afya,
kufanya utafiti na kutoa mafunzo kwa wafanyakaziwa kutoa huduma bora kwa
wananch.
Ameeleza hayo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la
msingi kwa majengo ya wodi ya watoto na wodi ya kutoa huduma za mama na mtoto
yaliyopo Mmanazi mmoja, ikiwa ni maadhimishio ya miaka 52 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Ujenzi wa wodi ya mama na mtoto inatarajiwa kugharimu euro milioni 9.9 itakayohusisha na vituo 19 vya
afya na kwa upande wa wodi ya watoto unatagharimu dola milioni moja nukta
6.7 za kimarekani ambapo Zanzibar imetoa nusu ya gharama ya mradi huo unategemewa
kumalizika mwakani.
Katika mealezo yake Rais Shein amesema ujenzi wa majengo hayo
ni moja ya hatua muhimu katika kutanua Hospitali ya Mnazi mmoja kuwa ya rufaa
ili kupunguza usafirishaji wa wagonjwa nje ya nchi hasa ya magonjwa wa figo na
saratani.
Ameishukuru Serekali ya Norway na Uholanzi kwa kuisaidia Zanzibar
kufanikisha mradi huo unaokwenda
sambamba na sera ya Mapinduzi iliyo asisiwa tokea 1964.
Nao Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Jaap Frederiks na wa Norway Hanne Marie Kaarstad wamesema wanaamini
kuwa mradi huo utaleta tija kwa wananchi wa Zanzibar kulingana na ongezeko la
idadi ya watu.
Hata hivyo wamewapongeza wananchi kuwa wastahmilivu mbali na
kuwepo changamoto za kisiasa ili wanaamini kuwa mzozo huo utaisha ili kufikia maamuzi
yanayosthiki huku wakiahidi kuendelea kusaidia Zanzibar katika mipango yake mbalimbali ya
meaendeleo.
0 comments:
Post a Comment