TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07
Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na
Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi,
kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.
Rais
Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa
ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya
hivyo.
Kwa
upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia
heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri
hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza
matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.
Jaji
Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli
kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya
ya madaraka na wizi wa mali ya umma.
"Lazima
kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya
rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia
hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini
watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
07 Januari,
2016
0 comments:
Post a Comment