January 11, 2016

Hatimaye, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ametoa msimamo wake na chama chake kufuatia mazungumzo ya siri ya kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika hotel ya kitalii ya Serena jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amesema hoja ya kurudiwa uchaguzi haina msingi kwani kunaweza kusababisha kutokea machafuko na migogoro  kwa uvunjifu wa sheria na katiba ya Zanzibar.
Amesema ni lazima maamuzi ya wanzibari na ustahmilivu wao waliouonesha baada ya mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kuchukuwa hatua hiyo ili kulete haki na si kuangaliwa maslahi ya viongozi wachache.
Maalim seif amevitaja vipengele kadha vya katiba alivyodai vimekiukwa na mwenyekiti wa ZEC Salimu Jecha na kumtaka ajiuzulu kwa kufuta matokeo kinyume cha sheria na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kukiuka katiba ya Zanzibar.
ameeleza kuwa anafahamu dhahiri kuwa kuna mpango wa kutangazwa tarehe Februari 28 mwaka huu kuwa ni ya kurudiwa uchaguzi ya lakini yeye pamoja na chama chake hawatakubali hilo.
Amesema tangu uchaguzi wa vyama vingi uanze Zanzibar umekuwa ukikubwa na kasoro kadhaa ukiwemo wa mwaka 2000 uliolazimu vituo 16 kurejea uchaguzi Zanzibar na hii ni kutokana na ZEC kuingiliwa kazi zake wakati haipaswi kupokea au kushinikizwa na chama chochote cha siasa au chombo chochote.
Aidha Maalim seif ambae ni mgombea wa urais Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF amemtaka rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kuongoza mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea Zanzibar kwa kufuata misingi ya kikatiba na sheria baada ya mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea na chini ya rais Dr Ali Mohamed Shein kwa kuwashirikisha marais wastaafu wa Zanzibar kutoonesha kuzaa matunda.



0 comments:

Post a Comment