TAARIFA
KWA UMMA
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi
ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza
katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia
na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.
Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda
kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya
mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na
Mshikamano wa Kitaifa.
Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016
0 comments:
Post a Comment