January 12, 2016

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameendelea kusisitiza suala kurudia uchaguzi na kutaka wananchi kuendelea kuishi kwa amani na utulivu huku wakisubiri Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi huo.
Amesema uchaguzi wa awali uliofanyika Novemba 25 mwaka jana ulifutwa na zec baada ya kubainika  kasoro kadhaa na uamuzi huo ulitangazwa katika gazeti la serikali na kueleza  kuwa  watangaza tarehe nyengine  baadae.
Dkt Shein amefahamisha kuwa kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar 1984 na sheria ya uchaguzi Zanzibar 1984 Tume ndio yenye jukumu la kusimamia uchaguzi wa rais madiwani na wawakilishi hivyo kufutwa kwa uchuguzi uko kisheria.
“ Tutarudi katika uchaguzi wa marudio ili wananchi watekeleza matakwa yao ya kikatiba kumtafuta kiongozi  halali  kwa kutumia mfumo  wa kidemokrasia.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo huko katika viwanja vya Amaan Zanzibar Dkt Shein amesisitiza wananchi kuendelea kuwa wastahmilivu, kuishi kwa amani na kuendeleza shughuli za maisha yao ya kila siku  na suala la uchaguzi wa Zanzibar lisiwe chanzo cha kuvunja sheria za nchi kwa makusudi
Amefahamisha kuwa suala la amani Zanzibar halina mbadala kwa vile limefanikisha kupatikana maendelo mbalimbali ya kijamii na taifa hivyo mwananchi wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kutii katiba  na sheria za nchi na serikali haitowavumilia watu wanaotaka kuharibu utulivu uliopo.
Rais wa Zanzibar amewomba viongozi wa wa seriali, wanasiasa, dini na wengine kuhakikisha wanatekeleza  wajibu wetu wa kuhamasisha  amani.
Akizungumzia kumekuwa na mafaniko kadhaa yaliyopatikana Zanzibar kipindi cha mwaka uliopita ambapo karibu miradi 31 inayogharimu zaidi ya dola milioni mia tatu imeanzishwa na mengine imeshaanza kazi.
Dkt Shein amesema Zanzibar imeadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi na yatendelewa kuenziwa sambammba na kudumisha Muungano wa Tanzania kwani ndio yaliyowezesha wananchi kuishi kwa amani na kupata maendeleo.



0 comments:

Post a Comment