January 12, 2016

Wazanzibari leo wanasherehekea miaka 52 ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964, yaliyoung’oa utawala wa Sultani kutoka Oman na kuwezesha wazalendo wengi kushika hatamu ya kuongoza nchi.
Katika kilele cha sherehe hizo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein atahutubia taifa katika uwanja wa Amaan.
Pia atapokea maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya Unguja. Matukio mengine makubwa yatakayofanyika katika uwanja huo ni Rais Shein kukagua gwaride la heshima la vikosi ya ulinzi na usalama, vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) .

Kwa mujibu wa taarifa sherehe hizo zitahudhuriwa na viongozi wa ngazi za kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano, John Magufuli

0 comments:

Post a Comment