April 05, 2014


 Tanzania imefanikiwa kupunguza matukio ya uhalifu kutokana wananchi kupokea  vyema dhana ya polisi jamii katika ulinzi na usalama wa nchi.

 Msaidizi Kamishna  wa polisi Zanzibar  Keneth Kaseke amesema  mpango huo wa ulinzi shirikishi umefanya jeshi hilo kufanya kazi kwa umakini zaidi kuwashirikisha moja kwa moja wananchi .

 Akizindua kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia ya Matemwe Kusini,  Mkoa wa Kusini Unguja amefahamisha kuwa mipango kadhaa iliyoanzishwa imeleta mabadiliko makubwa katika utendaji wa jeshi hilo wa kukabiliana na uvunjaji wa sharia.

Afisa Kaseke amekitaka kikundi hicho kufanya kazi kwa kufuata sheria za usalama  wa  nchi na kuacha kuchukuwa sheria mikononi mwao kwa wahalifu.

Amewataka askari polisi wa majimbo na wa shehia kutoa elimu zaidi ya dhana ya polisi jamii kwa viundi vya polisi  na wananchi ili kuweza kuteta mabadiliko zaidi katika kukabilina na uhalifu.

 katika hatau nyengine kikindi kimekabidhiwa vifaa vya kufanyia kazi za ulizni na usalama ikiwemo sare na viatu kutoka kwa wawekezaji wa mahoteli kitalii katika ukanda wa matemwe

.

0 comments:

Post a Comment