TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu
wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd
amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kuwa hali ya Zanzibar ni shwari na Wazanzibari wanasubiri kutangaziwa tarehe ya
kufanyika kwa uchaguzi.
Balozi
Seif Ali Idd ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 20 Januari,
2016 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.
"Mimi nimekuja kumpa taarifa juu ya hali yetu Zanzibar inavyokwenda,
nimemueleza kwamba Zanzibar ipo salama, Zanzibar ina utulivu na ina amani, nimeona
nije nimueleze kwa kuwa yeye ni kiongozi wetu"
alisisitiza Balozi Seif Ali Idd.
Makamu
huyo wa pili wa Zanzibar ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa amani na utulivu,
wananchi wa Zanzibar wanaendelea na shughuli zao kama kawaida tofauti na
inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
"Hayo
yanayoandikwa kwenye magazeti kuwa Zanzibar kuna fujo, Zanzibar kutatokea
machafuko sio kweli, na kama unavyojua uchaguzi ulifutwa na tume ya uchaguzi na
tunasubiri tarehe mpya ya uchaguzi itangazwe na tume ili tufanye uchaguzi"
amebainisha Balozi Seif Ali Idd.
Gerson
Msigwa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es
salaam.
20 Januari,
2016.
0 comments:
Post a Comment