January 21, 2016

Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Bw Ramadhan Kailima ametoa wito kwa serikali kurekebisha sheria ya uchaguzi ili kuwezesha kazi ya kuboresha daftari la wapiga kura kufanyika kila baada ya miezi sita au mwaka mmoja.
Amesema lengo lao ni kufanya hivyo ili kuhakikisha kila anaetimiza umri kusajiliwa pamoja na kupungua mzigo katika kipindi cha usajili kutokana na muda uliowekwa sasa
Alikuwa akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakaziwa tume hiyo jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa NEC jaji mstaafu Damian  Lubuva amesema moja ya changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu ulifanyika mwaka jana ni idadi ndogo ya wananchi  waliojitokeza kupiga kura  ikilinganisha na  ya waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura nchi nzima.
Ameeleza kuwa idadi ya watu waliojiandikisha walikuwa zaidi ya milioni 22 lakini ni milioni kumi na tano tu ndio waliopiga kura. Amefahamisha ingawa usimamizi wa uchaguzi uliopita ulikuwa na changamoto mbali mbali lakini ulimalizika kwa   amani na utulivu na amewaomba wadadu mbali mbali  kujitokeza kutoa  elimu zaidi ya upigaji kura.
Nae Mkurugenzi wa NEC Kailima Ramadhan Kailima amesema lengo lao ni kukusanya sheria zote zinazohusiana na uchaguzi  na kuzifanyia marekebisho  ili kufanya uandisha wa piga kura angalau kila mwaka  ikifika mwaka 2020 zoezi hilo liwe limekamilika ukilinganisha na mwaka jana ambapo vifaa vilichelewa kufika kwa wakati.

0 comments:

Post a Comment