Serikali imewaagiza maafisa wa afya nchini kuhakikisha kila
kaya inakuwa na choo bora ikiwa ni hatua ya
kuhakikisha jamii inaupekana na magonjwa yanayotokana
na uchafu mazingira.
Mpango huo pia unalenga kwenda
sambamba na suala la usafi wa mazingira kuwa
endelevu kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando, wakati wa mkutano wake na waandishi wa
habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara
hiyo.
Katibu Mkuu huyo alieambatana pamoja na baadhi ya viongozi wa
Ofisi ya Makamu wa Rais na ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuzungumzia kuhusu usafi wa
mazingira katika kuadhimisha siku ya Uhuru ya Desemba 9, mwaka 2015, ugonjwa wa kipindupindu
na polio.
“Wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa kutekeleza agizo hili kwa
kujiwekea utaratibu wa kufanya usafi maeneo yao,” amesema Dkt. Mmbando.
Amesema ugonjwa wa kipindupindu pamoja na magonjwa mengine
yanayohusiana na uchafu huenea kwa kasi kutokana na hali duni ya usafi katika
maeneo tunayoishi.
Takwimu zinaonesha kuwa kati ya taka ngumu zinazozalishwa ni asilimia
50 tu huzolewa na kupelekwa dampo na kiasi cha taka kinachobaki huzagaa katika
maeneo mbalimbali hasa kando kando ya barabara, katika maeneo ya kukusanyia
taka (Collection points), chini ya madaraja na katika maeneo ya wazi na
kubabisha miji kuonekana michafu.
Pia kiasi asilimia 34 ya
kaya ndizo zenye vyoo bora na asilimia
12% hazina vyoo kabisa hali inayohatarisha afya ya jamii na kusababisha kuenea
kwa urahisi kwa magonjwa ya kuambukiza.
Dkt amewataka watendaji hao, kusimimia suala hilo kwa kuzingatia
sheria za afya zilizopo, huku akizitaka halimashauri na mamlaka kuweka
sheria ndogo ndogo ili kutekeleza agizo hilo Rais kwa vitendo.
Akizungumzia shughuli za usafi katika siku hiyo ya Uhuru
amesisitiza kuhamasishwa jamii kwa njia mbalimbali ili kujitokeza kwa wingi katika
maeneo yao na sehemu za kazi au biashara, vyombo vya usafiri wa abiria na vituo
vya wasafiri kwa kushirikisha wadau mbalimbali ikiwa juhudi za kupambana na
kipindupindu.
Tayari
Mikoa mingine 20 imeathirika na ugonjwa huo ulio ibuka kwa mara ya Agosti15, 2015
katika mkoa wa Dar es Salaam na takwimu zinaonesha watu 9,906 walipata
ugonjwa huu na kati yao jumla ya watu 149 wafariki dunia
na wagonjwa wengine wamepata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani hadi tarehe
2 Desemba, 2015.
Magreth Kinabo- MAELEZO DSM
0 comments:
Post a Comment