December 04, 2015


WATUHUMIWA nane wa upotevu wa makontena 349 yaliyovushwa Bandarini ya Dar es Salaam bila kulipiwa kodi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na Kamishna wa Kodi na Forodha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki
Washitakiwa wote wamerudishwa rumande hadi tarehe 17 Desemba kwa kuwa  mahakama hiyo haina uwezi wa kusikiliza  wala  kutoa dhamana ya keshi hiyo.

0 comments:

Post a Comment