Madiwani na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Magharibi wametakiwa kuongeza kasi ya kiutendaji kufikia malengo ya maendeleo pamoja na kuwa na ari katika ukusanyaji mzuri wa mapato.
Afisa sheria kutoka Wizara ya nchi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na idara maalum Zanzibar, Zainab Khamis Kibwana amesema mapato ya uhakika katika halmashauri yanafanikisha utekelezaji wa haraka miradi ya maendeleo kuwafikia wananchi sambamba na kutekelezwa kwa wakati.
Afisa Zanab alikuwa akifungua kikao cha cha baraza la madiwani cha kupitia taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi 9 kutoka Julay 2013- hadi March 2014 pamoja na makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2014-2015.
Amesema katika kuhakikisha mapato ya leseni yanapatikana kwa uhakika ni lazima halmashauri hiyo kufanya utafiti wa kujua hali halisi ya wafanyabiashara jambo litakaloweza kuwa na mipango bora wa utaoaji wa leseni kwa mujibu wa ukubwa wa biashara husika.
Nao viogozi hao wamesisitiza ushirikiano kati ya watendaji na madiwani katika kusimamia upotevu wa mapato yanayochangia kutofikia makadirio yanayowekwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2014-2015 imekadiria kukusanya jumla ya shilingi milioni mia tisa hamsini ambapo kipindi cha mwaka wa fedha 2013-2014 na hadi kufikia march imeshakusanya zaidi ya shilingi milioni miatano thalasini saba
0 comments:
Post a Comment