April 09, 2014


zenjkijiwe.blogspot.com
sehemu ya kutangazia ya redio noor iliyoteketea na moto
Kituo cha Redio cha Al-Noor fm kilichopo Mtoni Kidatu wilaya ya Magharibi Unguja kimeteketea moto usiku wa kuamkia leo (jumatano)  na kusababisha hasara  inayokadiriwa kufikia shilingi milioni 80.
Mtangazaji aliyeakiendesha vipindi  Abubakar Fakihi amevunjika mguu na mkono baada ya kuchupa kutoka afisi za studio hiyo iliyopo ghorofa ya kwanza katika jengo la msikiti nour akijaribu kuokoa maisha yake.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kituo hicho Mohammed Suleiman ameeleza kuwa huenda moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme ila uchunguzi unaendelea kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo.

Mkurugenzi huyo amesema moto huo umezuka baada ya kurudi umeme uliokuwa umezimwa kwa wakati huo.
Amefahamisha kuwa moto huo umeteketeza maeneo yote ya studio tatu ikiwemo ya kurushia matangazo na vitu mbalimbali ikiwemo transmita, kompyuta, mafeni,mazulia na vitu vyengine
Baadhi ya waandishi waliotembelea Hospitali kuu ya Mnazimmoja, walishindwa kumuona mtangazaji Abubakar Fakih kwa taarifa kuwa alikuwa bado anaendelea na matibabu katika chumba cha upasuaji.

Hii ni mara ya pili kwa kituo cha Redio Nour fm kuungua moto na kusababisha hasara kubwa

zenjkijiwe.blogspot.com/
Mkurugenzi wa Redio Noor fm Mohamed Suleiman akizungumza na waandishi juu ya tukio la kuungua moto studio za redio hiyo
zenjkijiwe.blogspot.com
baadhi ya vifaa vya redio Noor vilivyotekea kwa moto
zenjkijiwe.blogspot.com
Mtangazaji Aboubakar Fakihi aliyejeruhiwa katika ajali hiyo

0 comments:

Post a Comment