April 08, 2014


MAMLAKA ya vitmbulisho vya Taifa (NIDA) imewataka  viongozi wa vyama vya siasa wa Wilaya ya  Mkoani kuwaelimisha wananchi  kwa kufuata maelekezo ya uwandikishaji wa vitambulisho  vya Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea vituo vya uandikishaji katika Wilaya hiyo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA  Tomas William amesema   baaadhi ya viongozi hao  wanatoa taarifa zisizo sahihi za Mamlaka hiyo na kuwafanya baadhi ya wananchi kutotiliana maanani juu miongozo inayohitajika .
Nae Afisa Habari wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Said Mohammed Said amesema  utaratibu  uliyouwekwa na Mamlaka ya vitambulisho  juu ya vielezo vya uandikishaji ni kupata taarifa sahihi  ya mwananchi kwa kuepusha  migogoro na 
wananchi. 
Baadhi ya Masheha  wamesema licha ya kuwepo kusoro ndogo ndogo  zinazojitokeza baadhi ya wananchi zoezi hilo linaenda vizuri .
Uandikishaji huo umeanza tarehe 5 mwezi huu na utachukuwa  wiki sita katika shehia za mikoa yote ya Pemba.
zenjkijiwe.blogspot.com
Mkufunzi Bi Shifaa Said akielezea juu ya kuripoti taarifa bora za masuala ya jinsia .

0 comments:

Post a Comment