Mkuu wa Mkoa wa kusini unguja Dr Idrisa Muslim Hija |
Mkuu wa Mkoa wa kusini Dr Idrisa Muslim Hija
amesema uhakika wa upatikanaji wa rasilimali za bahari kwa faida ya jamii
unahitaji usimamizi bora ili kudhibiti uharifu wa mazingira ya maeneo ya ukanda
wa pwani .
Akizungumza na wadau wa maendeleo wa maeneo hayo yana rasimali
nyingi zinaweza kutumika kama njia kuu za kuendesha maisha ya wananchi na
kuleta maendeleo ya taifa.
Hata hivyo amesema mafanikio hayo hayawezi kufikiwa iwapo
hakutakuwa na matumizi na usimamizi madhubuti wa rasilimali hizo na matumizi
yake kwa faida ya jamii..
Dr Hija ameitaka jami ya ukanda huo kuweka utaratibu bora
utakaoweza kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali hizo na kuongeza uhifadhi
utakaopelekea wavuvi kupata maslahi bora kupitia kazi yao.
nae Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya uvuvi Mussa Aboud
Jumbe ameeleza amesema wanafanya utafiti ili kugundua matatizo ya mabadiliko ya
tabia nchi na athari zake kwa lego la kuangalia uwezekano wa kutafuta njia bora
itakayosaidia wananchi na serikali kwa pamoja.
Mkutano huo umeandaliwa na idara ya uvuvi na Benki ya dunia
kupitia mradi wa uvuvi kusini mashariki mwa bahari ya hindi (SWIOFISH)
ili kuandaa makubaliano ya kuanzisha mradi wa kuisaidia jamii ya ukanda wa
bahari.
0 comments:
Post a Comment