Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi |
Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi ameiagiza Wizara ya Elimu na uongozi wa
Wilaya ya Micheweni kushirikiana na Walimu wa skuli ya Msuka kudhibiti utoro wa
wanafunzi katika Skuli hiyo.
Agizo hilo
amelitoa alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Elimu Wilaya , Walimu ,
Kamati ya Skuli na Wanafunzi wa Skuli hiyo baada malamiko ya wanafuzi kutoroka
skuli siku ya Ijumaa bila ya sababu maalum.
Imeelezwa kuwa zaidi ya wanafunzi 200 kati ya
wanafunzi 363 hutoroka skuli siku hiyo.
Dadi ameeleza kuwa kitendo hicho cha wanafunzi kujipa mapumziko kinyume na utaratibu hakiwezi kufumbiwa macho kwani ni kinyume na utaratibu.
Hivyo ameitaka kamati ya skuli hiyo ya Msuka kushirikiana na viongozi wao kwa nguvu zote na kutaka hatua za kinidhamu kuchukuliwa kwa wanafunzi wenye tabia hiyo.
Mapema
Afisa Elimu Wilaya ya Micheweni Mbwana Shaame Said amesema tatizo hilo linalochangiwa na wazazi kutokuwa tayari
kufuatilia maendeleo ya masomo ya watoto wao. Dadi ameeleza kuwa kitendo hicho cha wanafunzi kujipa mapumziko kinyume na utaratibu hakiwezi kufumbiwa macho kwani ni kinyume na utaratibu.
Hivyo ameitaka kamati ya skuli hiyo ya Msuka kushirikiana na viongozi wao kwa nguvu zote na kutaka hatua za kinidhamu kuchukuliwa kwa wanafunzi wenye tabia hiyo.
Hata hivyo amesema wameandaa mkakati wa kukutana na wazazi kujadiliana kutafuta hatua za kuchukuwa za kukabiliana na hali hiyo inayodidimiza maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka kwa Walimu wa Skuli hiyo Siku ya Ijumaa wanafunzi wengi katika Skuli hiyo hawahudhuri masomo yao ambao wametaka Serikali ya Mkoa isaidie katika kutafuta suluhisho la kitendo hicho.
0 comments:
Post a Comment