Vyombo vya habari vimeshauriwa kuweka sera na
miongozo ya masuala ya jinsia ili kuenda sambamba na harakati za utekelezaji wa
mkakati wa mapambano ya masuala tanzania.
Mshauri wa taasis ya jinsia vyombo vya habari na
jisia katika nchi za Kusini mwa Afrika GEMSA Gladness Hemed
Munuo Amesema ni muhimu kwa vyombo hivyo kuwa tayari kuchukuwa juhudi hizo
kutokana na umuhimu wa masuala hayo kwa maendeleo yanayohusu watu wote na si
wanawake pekee .
Amefahamisha kuwa utafiti kuhusu vyanzo vya habari
katika nchi za ukanda wa Afrika Kusini 2012 umeanisha wanawake wametumiwa kwa
asilimia 16 pekee katika taarifa zote zilizotolewa.
Bi Gladnes Ameongeza kuwa GEMSAT iko tayari kutoa msaada kwa ajili ya kuandaa
makakati huo ambapo teyari karibu vyombo vya habari 10 vimeshaandaa muongozo wa
masuala ya jinsia.
Akitoa ufafanuzi mkufunzi wa mafunzoo hayo salim
said salim amesema wakati umefika kwa taasisi zinazosimamia utaoaji leseni za
utangazaji kwa vyombo vya habari kuweka msisitizo wa masuala ya jinsia kuwa ni
moja ya masharti ya kupata leseni.
0 comments:
Post a Comment