Wasanii kisiwani pemba wametakiwa
kutumia vipaji vyao katika kuelimisha jamii dhidi ya kujikinga na madawa ya
kulevya na ukimwi ili kupata vijana bora wanaoweza kulitumikia taifa.
Afisa Afisa Tawala Wilaya ya Mkoani
Abdalla Salim Abdalla Amesema iwapo wasanii watachukuwa nafasi yao ya
kuielimisha jamii mambukizi ya maradhi ya ukimwi na matumizi ya dawa za kulevya
yatapungua kwa kiasi kikubwa
Ametoa wito huo alipokuwa akifungua
mafunzo ya kupambana na maradhi ya ukimwi na madawa ya kulevya yaliyo
washirikisha wasanii wa pemba.
Afisa huyo meipongeza jumuia ya zayadesa
kwa kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha vijana kujiepusha na maradhi ya
ukimwi na madawa ya kulevya jambo linaloweza kusaidia kupunguza ongezeko la
matatizo hayo nchini.
Amesema ya ukimwi Zanzibar yamefikia
asilimia moja jambo ambalo ni hatari kwa vijana wa Zanzibar ambao ambao ni
nguvu kazi ya kufanikisha harakati za maendeleo.
Nae Mratibu wa Zayadesa Zanzibar Mgoli
Lusiana amesema taluma ya mapambano dhidi ya ukimwi na madawa ya kulevya
yanahitajika kuongezwa kasi zaidi ili kuwafikia vijana wengi zaidi.
0 comments:
Post a Comment