Jeshi
la polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limeannzisha mradi wa kuhamasiha kupunguza matokeo
ya uhalifu katika familia na jamii.
Kamanda polisi mkoa huo Mkadamu Khamis
Mkadamu amesema lengo la mradi huo ni kuisaidia jamii kufahamu umuhimu wa kuimarisha
mifumo ya malezi bora ambayo ni njia pekee salama ya kuzuia ukuaji wa uhalifu.
Amefahamisha kuwa mradi huo wa familia yetu hamna uhalifu umezingatia kwa kuwa
wengi wa wahalifu wenye umri mdogo familia zao hazikuzingatia malezi bora
pamoja na uslama watoto wao.
Akizungumzia kuhusu operesheni za kukamata wahalifu ameeleza kuwa jumla watu
kumi na saba wamefikisha mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo utimiaji wa
dawa za kulevya na kufanya biashara haramu ya pombe ya kienyeji.
Kamanda Mkadamu ameongeza kuwa jeshi hilo linaendelea kufanya operesheni ya
pamoja na wananchi wa shehia mbalimbali kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama
ndani ya mkoa wa mjini Magharibi.
0 comments:
Post a Comment