Ukosefu utoaji huduma bora, gharama na watendaji
wasiokuwa na ujuzi imesababisha sekta ya
utalii kupungua mapato yake.
Mkurugenzi Mtendaji taasisi inayotoa huduma za utalii Tanzania ya Travelport
Elisaph Mathew amesema matatizo hayo yamesababisha kupungua idadi ya watalii kutembelea
nchini ikilinganishwa na wanaingia katika nchi wanachama wa jumuiya
ya afrika mashariki.
Elisaph Elisaph Mkurugenzi mtendaji travelport tanzania |
“Uganda wametembelea watalii laki tisa, Kenya milioni
moja na laki mbili wakati Tanzania imetembelewa
na wageni laki nane wakati imebarikiwa kuwa na vivutio vingi ila inapata
malalamiko tu ju ya utoaji huduma mbaya kwa watalii…” amefahamisha.
Akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti kwa
wahitimu wa mafunzo ya utoaji wa huduma za usafiri katika sekta hiyo kwa njia ya elektronic
amewataka wadau wa sekta hiyo kuacha kufundisha watendaji wao kiholela ili kupata
watendaji watakaofanya kazi kwa ufanisi.
nae mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Zenith Tours and
travel Salim Mohamed Suleiman amesema Zanzibar imepata nafasi nzuri katika
kukuza sekta ya utalii na kufikia viwango vya kimataifa katika utoaji wa huduma
kwa watalii.
Mafunzo hayo utoaji wa huduma kwa njia ya elekrtonic
ni ya kwanza Zanzibar yametolewa kupitia kampuni ya Zenith kwa ushirikiano na
kampuni ya Travel port yenye matawi zaidi ya 150 duniani
0 comments:
Post a Comment