Umoja wa taasisi mbalimbali za
kiraia Tanzania (AZAKI) umesema watanzania hawajapendezwa na vitimbi na maneno
ya kashafa ya wajumbe wa bunge la katiba huku
fedha za umma zikipotea pasipo na jambo la maana.
Katika taarifa yao ya pamoja juu
ya mjadala wa katiba unaoendelea huko Dodoma kuwa wajumbe hao wamepoteza utaifa na badala yake
wamejikita kwenye ubaguzi,ubabe,vijembe na vitisho vya kutoheshimiana kinyume
na matakwa ya mkutano huo.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini dar es salaam
mwenyekiti wa umoja huo Irenei Kiria amesema
taasisi hizo zimehuzunishwa na tabia ya kudhihaki na kudhara rasimu ya
pili ya katiba pamoja na tume ya katiba na hasa Mwenyekiti wake Jaji Warioba, aliyekusanya maoni ya wananchi kuhusu
uundwaji wa katiba mpya.
Amefafanua kuwa inasikitisha mwenendo
wa mijadala ya bunge hilo inaelekea
kutetea maslahi ya watakwa na vyama siasa na makundi binafsi badala ya maslahi
ya ya taifa na ustawi wa wananchi inayosababisha masuala madogo kuchukuwa muda
mrefu kitendo kinachotakiwa kutofumbiwa macho.
Umoja wa asasi hizo zipatazo 500 za Tanzania umewasihi
wajumbe wa bunge maalum la katiba pamoja na uongozi wa bunge hilo kurekebisha
kasoro zilizoorodheshwa na na taasisi hizo ,ili kupata katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi
wenyewe na si kuhatarisha amani ya nchi
0 comments:
Post a Comment