April 18, 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amepokea tuzo ya utumishi bora kwa nchi za Afrika kutoka taasisi ya Afrika Magazine ya mwaka 2013.Akizungumza na waandishi wa habari ikulu Jiji Dar es salaam baada ya kupokea tuzo hiyo. Amesema tuzo hiyo ni ya watanzania wote kwa vile nao wametoa ushrikiano wao katika kutekeleza mambo mbalimbali ya Tanzania yaliyofahamika duniani.
Rais Kikwete amewaomba watanzania kushirikiana pamoja ili kuleta  maendeleo ya nchi .Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Benard membe aliemwakilisha Rais kupokea tuzo hiyo nchini Marekani.Tuzo hiyo ni mara ya tatu kutolewa kwa nchi za afrika na iliwahi kutolewa kwa nchi za algeria na Sera leone.
                                                                                                                                 

Baadae Rais Kikwete alikwenda kutoa heshima za mwisho katika msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani  huko Kibada jijini Dar es salaam leo kwa kutumia pantoni
 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowahani na kutoa heshima za mwisho katika msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani  huko Kibada jijini Dar es salaam leo

0 comments:

Post a Comment