April 17, 2014

zenjkijiwe.blogspot.com
Waziri wa nchi afisi
 ya Makamu wa pili wa rais
Mohamed Aboud
Utekelezaji wa mpango umoja wa forodha kwa nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki umeharakisha  ukuaji wa uchumi kwa nchi za ukanda huo.
Waziri wa nchi afisi ya makamu wa pili wa rais mohamed aboud amesema imefanikiwa kutokana na  sera utekelezaji wa itifaki hiyo kutilia mkazo wa kubuni miradi ya kuwawezesha wananchi kusambaza bidhaa zao na kupatikana  kwa soko la uhakika
Waziri Abod akizungumza katika kongamano la jumuiya afrika mashariki ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Amesema mafaniko hayo yanaharakisha maendeleo ya nchi wanchama na kufikia mikakati ya kupunguza  umasikini.
Akitoa mada katika kongamano hilo Mkurugenzi Msaidizi wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dk Abdalla Makame amezitaka  sekta binafsi kuendelea kuitetea jumuiya  ya afrika mashariki ili kuendeleza maslahi ya nchi wanachama.
Jmuiya ya afarika mashariki inazijumuisha nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi amapo moja ya lengo lake ni kuimarisha maeldelo ya kiuchumi na utengano wa wananchi wa nchi hizo.

0 comments:

Post a Comment