April 17, 2014

zenjkijiwe.blogspot.com
Afisa habari Mkuu wa polisi Zanzibar
Inspekta, Mohamed Mhina  
Jeshi polisi Zanzibar limesema limejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa Amani katika kipindi chote cha sikukuu ya pasaka.
Afisa habari Mkuu wa jeshi hilo Inspekta, Mohamed Mhina  amesema wameshawaagiza makamanda wa mikoa ya    Unguja na Pemba kuimarisha Ulinzi na Usalama katika maeneo ya  ibada ya waumini wa Kikiristo.
Amesema jeshi hilo limelazimika kutoa agizo hilo ili kuhakikisha maeneo yote yatakayotumika kwenye  mkesha  wa  ibada hiyo yanafanyiwa doria pamoja na sehemu zote mijini na vijijini ili waumini wa dini ya   ili kuepusha uvunjifu wa amani .
Inspekta Mhina amewaomba wananchi kutoa ushirikiano na kutoa taarifa mara watakapobaini dalili za uvunjaji wa sheria au kupanga uhalifu  katika maeneo yao.
Ametoa taarifa hiyo vyombo vya habari kwa niaba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame katika kuelekea sikukuu ya pasaka.

0 comments:

Post a Comment