TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa tisa
wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
umemalizika katika ngazi ya wataalamu mjini Zanzibar
Mkutano wa Baraza la kisekta la Mawaziri wa Afya la Jumuiya ya
Afrika Mashariki unafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 14 hadi 17 Aprili, 2014.
Mkutano huo ulianza katika ngazi ya wataalam tarehe 14 hadi 15 Aprili 2014,
ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 16 April 2014 na kuhitimishwa na ngazi ya
Waheshimiwa Mawaziri tarehe 17 Aprili, 2014.
Pamoja na mambo mengine
Mkutano huu umepitia taarifa ya utekelezaji wa maamuzi na maagizo mbalimbali ya
Mikutano iliyopita na pia kujadili masuala ya kukamilisha kwa Mpango Mkakati
wa Sera ya Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,Itifaki ya Afya ya Jumuiya
,kujenga sekta ya rasilimali watu ya Afya ya magonjwa yanayoambukiza na
yasiyoamabukiza, haki, jinsia na afya ya uzazi.
Mkutano huo ulifunguliwa na
Bi. Asha Ali Abdallahi, Katibu Mkuu ,Wizara ya Uwezeshaji, Jamii, Vijana
na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye alizitaka Nchi
Wanachama wa Jumuiya kuweka pamoja na kuimarisha sera muhimu kwa
ajili ya kuendeleza na kukuza hali ya maisha kwa wananchi wa Afrika Mashariki.
Naye Mkurugenzi wa Sekta za
Kijamii wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki akiongea na wataalamu wa
Mkutano huo alisema kuwa Sekretarieti ya Jumuiya inatumbua Juhudi za wataalamu
hao kwa mchango wao mkubwa katika kuendeleza mtangamano wa Afrika Mashariki.
Aidha Kiongozi wa ngazi ya
wataalamu kwa upande wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Elias M. Kwesi
aliwakikishia ujumbe wa mkutano namna Tanzania ilivyo makini katika utekelezaji
na uendelezaji wa Mtangamano na kuwataka wajumbe wa mkutano kwa pamoja
kutekeleza sera na mikakati ya kupambana na magonjwa yayoibuka hususani ikiwemo
kitisho cha magonjwa yasiyo ambukiza.
Mkutano huu kwa sasa
unaendelea katika ngazi ya makatibu wakuu na utaitimishwa katika ngazi ya
Mawaziri.
IMETOLEWA
NA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
0 comments:
Post a Comment